-->

Ney wa Mitego Awekewa Ulinzi Zanzibar

MKALI wa wimbo wa ‘Wapo’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, amesema tangu alipotoa wimbo wa ‘Wapo’ amekuwa akifanya shoo zake katika  mikoa mbalimbali akiwa na ulinzi wa kutosha.

Mlinzi huyo kabla ya kuwasili visiwani Zanzibar kwenye tamasha la Muziki na Utamaduni la Zanzibar Swahili, alikubaliana na waandaaji wa tamasha hilo wampatie ulinzi wa kutosha na hoteli yenye ulinzi wa kutosha kwa kuwa bado ana hofu na maisha yake.

“Tangu nilipokamatwa na polisi kutokana na wimbo wangu wa ‘Wapo’, nimekuwa nikifanya shoo zangu nikiwa na ulinzi wa kutosha kwa kuwa bado najiona nahitaji kulindwa maana peke yangu sitaweza.

“Hata kwenye onyesho lango la juzi usiku kule Singida na Jana Zanzibar, niliwaomba kabisa waandaaji wanipatie walinzi wa kutosha ingawa nami nina walinzi wangu siku hizi,” alisema Nay wa Mitego.

Hata hivyo, viongozi wa tamasha hilo walisema walimpatia mabaunsa wawili na askari polisi mmoja kwa ajili ya kumlinda mwanzo hadi mwisho wa shoo yake baada ya msanii huyo kuomba apatiwe ulinzi kwa viongozi hao.

“Ney alituomba ulinzi alisema anataka apatiwe mabaunsa wawili na askari polisi mmoja, nasi tumefanya kama alivyotaka maana lipo katika makubaliano yetu kwa ajili ya shoo yetu,” alieleza Meneja wa Tamasha hilo.

Ney aliongeza kwamba baada ya shoo yake kwenye tamasha hilo ataanza ziara ya mikoani kuutangaza wimbo wake wa  ‘Wapo’ ambapo ataanza na mkoa wa Iringa na Arusha kisha mikoa mingine 11.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364