Ney wa Mitego Awekwa Mtegoni, Akamatwa
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limethibitisha kumkamata na kumshikilia rapa wa muziki wa kizazi kipya, Emanuel Elibariki maarufu Nay Wa Mitego leo usiku mjini Morogoro.
Akizungumza na Mwananchi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha kumkamata rapa huyo kwa kosa la kutoa wimbo unaoikashifu serikali.
“Alikamatwa saa nane usiku wa leo, kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya Serikali na shauri lake lipo Dar es Salaam kwa sasa, atapelekwa kuhojiwa kuhusiana na masuala yake ya kazi zake za sanaa kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa,” alisema Kamanda Matei.
Mwananchi