-->

Ney wa Mitego: Diamond, Kiba Hawanitishi

MKALI wa muziki wa hip hop Tanzania, Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’, amesema hazimwi na bifu la Dimoand na Ali Kiba, huku akiweka wazi kuwa yeye hana mpinzani hapa nchini katika aina ya muziki anaoufanya.

Akizungumza jana alipotembelea ofisi za Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Rai na Dimba, Ney alisema ushindani uliopo kati yao haumtishi kuachia nyimbo zake kwa kuwa hajawahi kufunikwa.

Rapa huyo anayetamba na video ya wimbo wake mpya wa ‘Makuzi’, alisema hawezi kufunikwa kutokana na ubunifu wake.

“Mimi sina mpinzani katika muziki wangu ndio maana sijahofia kutoa wimbo kwenye kipindi hiki ambacho Diamond na Kiba wapo kwenye upinzani mkubwa, ninaamini upinzani wao unachangamsha muziki, lakini hawanitishi,” alisema Ney.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364