Nikki Mbishi Arusha Dongo kwa Nikki wa Pili
Msanii wa Hip Hop Nikki Mbishi amemchana Nikki wa Pili na kumuambia kwamba aache kujiita msemaji wa wasanii kwa kuwa yeye ni msemaji wa kikundi kidogo cha wasanii wachache.
Akiongea kupitia eNewz Nikki amesema Nikki wa Pili hapaswi kujiita msemaji wa wasanii kwa kuwa sanaa ya muziki ipo huru na kila mmoja anaposema ni msemaji wa wasanii siyo sahihi kwa kuwa hajui mambo ambayo wasanii wengine wanayawaza vichwani lakini pia hajachaguliwa na mtu kuwa msemaji wa wasanii.