-->

Nikki wa Pili Awaasa Mafisadi, Awakumbusha Kifo

Msanii Nikki wa pili ambaye pia ni mwanazuoni anayetoka kundi la Weusi ambalo linafanya vizuri kwenye muziki wa Hip Hop, amewaasa mafisadi juu ya wanachokifanya, huku akiwaonya kuwa maisha bado yatakuwa yale yale hadi siku ya kifo.

niki-wa-pili03

Kwenye ukurasa wake wa instagram Nikki wa Pili ameandika ujumbe akiwakumbusha watu wanaopenda kujilimbikizia pesa, kuwa hata uwe na pesa nyingi kiasi gani, bado kuna vitu vitalingana na yule asiyenacho, hivyo ni muhimu kuwafikiria na wengine’

“Unafedha nyingi…unaweza kuwa na jumba la kifahari vyumba sita…lakini ukilala unalalia kitanda kimoja kama watu wengine,
unaweza nunuwa lory la mchele…lakini ukila utakula sahani moja kama wengine, waweza nunua duka zima la nguo….lakini ukivaa utavaa suruali moja kama wengine, sasa kuna haja gani kufisadi au kuzulumu jasho la wengine na kuacha wengine wakikosa kitu…ulivyo jilimbikizia wewe”, aliandika Nikki wa Pili.

Nikki wa Pili aliendelea na waraka huo huku akiwakumbusha siku ya mwisho ya maisha na juu ya kifo ambacho kila mmoja atakipitia.

“Kataa kupora jasho la wengine….kumbuka watu kama hao siku ya umauti hali huwa mbaya….kutoka roho waweza piga mpaka sarakasi ya uchungu…..#tukatae mwanadamu mwenzetu kulala bila kula”, aliandika Nikki.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364