Nilimtoa Masogange-Belle 9
Msanii wa RnB Abednego Damian ‘Belle 9’, amesema umaarufu wa mkali wa kunogesha video za wasanii, Agnes Gerald ‘Masogange’, umetokana na wimbo wake wa ‘Masogange’.
Belle 9 alisema huwa anaamini kipaji cha mtu ndio maana wengi aliowashirikisha katika nyimbo zake wamepata umaarufu mkubwa.
“Nimefanya kazi na wasanii wasiotambulika akiwemo Masogange na wamepata umaarufu mkubwa pia nimefanya kazi na maprodyuza wengi wasiojulikana lakini baada ya kazi hizo wamejulikana, hivyo huwa sidharau uwezo wa mtu ninachoangalia ni ubora wa kazi zake na si jina lake hata kama ni chipukizi,” alisema.
eatv.tv