-->

Ommy Dimpoz Agoma Kuzungumzia Ishu ya Mama Diamond (Video)

Msanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz amesema hawezi  kuzungumzia ishu ya post ya mama mzazi wa Diamond katika ukurasa wake wa Instagram.

Ommy Dimpoz

Muimbaji huyo amesema kufanya hivyo ni kuamsha hisia upya kwa mambo ambayo yalishapita na hata menejimenti yake imemkataza kuzungumzia suala hilo.

Katika exclusive interview na Bongo5 Ommy Dimpoz amesema asingependa kuzungumzia hayo lakini kikubwa anachoweza kusema ni kwamba mavuguvugu lazima yawepo kwani ndio kuchangamka kwa muziki na ukizingatia Bongo Flava siyo kama kwaya.

“Hayo mengine yanayotokea is just a game lakini siyo vitu vya kushikana mashati au kumwagiana tindikali, hatujafikia huko ila ukiangalia industry zote duniani hayo mambo yapo na vinachagia wanamuziki kuumiza vichwa zaidi,” amesema Dimpoz.

“Tukiongea tunakuwa tunarudisha hayo mambo tena nyuma, mimi mwenyewe sasa hivi hata menejimenti imesema bwana hayo mambo husizungumzie tena.  Hayo mambo tukizungumza tutaamsha hisia, inakuwa haijakaa sawa, nafikiri yaliyopita yamepita,” ameongeza.

Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Cheche’ aliingia katika vita kali ya maneno mtandaoni mara baada ya kuposti picha akiwa na mama mazazi wa Diamond na kuweka maelezo ambayo yalileta utata mkubwa na kukosolewa vikali, hata hivyo posti hiyo ilikuja kufutwa baada ya muda.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364