-->

Ommy Dimpoz Kuwashangaza Mashabiki Wake

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema anajipanga kufanya kitu kitakachowashangaza mashabiki na wadau wa muziki nchini.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ommy Dimpoz alisema hawezi kuzungumza sana kitu alichokiandaa kukifanya hivyo mashabiki wasubiri.

“Ninajipanga kuwashangaza mashabiki zangu, wajiandae kusikia kile nitakachokifanya, nimekuwa nikisafiri mara kwa mara wakati huu ambao nipo kimya, nimefanikiwa kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vimefumbua akili yangu,” alisema Dimpoz.

Alisema mashabiki wamekuwa wakilalamika na kudai amefulia, jambo ambalo halina ukweli wowote kwani kila kitu kinafanyika kwa mipango.

Alisema kuwa kimya kwa muda mrefu si sababu ya kufulia au kushindwa kuendelea na fani kama ambavyo mashabiki wengi wamekuwa wakisema.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364