-->

P-Funk Majani Atoboa Siri ya Kupumzika Muziki

Mkongwe katika utayarishaji wa muziki bongo, P. Funk Majani ameweka wazi chanzo cha kupumzika kwa muda mrefu katika uandaaji wa muziki wa bongo fleva ni maslahi madogo ambayo hayakuwa na manufaa kwenye maisha yake.

Majani amefunguka hayo kwa mara ya kwanza ndani ya Planet Bongo ya East Africa radio na kusema kwamba alilazimika kuachana na muziki baada ya kuona anatumia nguvu nyingi huku watu wengi wakitajirika kupitia nguvu zake huku yeye akibaki mtupu.

“Niliacha kutengeneza muziki kwa muda kidogo kwa sababu nilijikuta na control industry nzima ya muziki  alafu pesa sipati, maisha yangu yakawa hayabadilik, Kujenga nyumba ilikuwa tunachukua miaka na miaka kuzimalizia kwa sababu hela ni za kuunga unga hapo hapo unaona wenzako wanapiga pesa ndefu ikabidi nifanye uamuzi wa kupumzika niangalie kipi cha kufanya – alifunguka Majani.

Hata hivyo Majani baada ya kurudi kwenye game amesema kwamba ujio wake atashirikisha wasanii wachache sana kwenye kufanya nao kazi huku akibainisha kwamba mpaka sasa tayari ana wasanii wasiozidi saba anaofanya nao kazi.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364