Peter Msechu Alia Ukata
Msanii Peter Msechu ambaye mara nyingi amekuwa akilalamikia hali ya ukata katika maisha yake, leo amefunguka tena na kusema kuwa yupo tayari hata kufanya show ya kuwaimbia kuku, ili mradi aingize pesa.
Kitendo hicho kimeongeza mashaka juu ya mkwanja wanaoingiza wasanii, mpaka kufikia hali mbaya kiuchumi.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East AFrica Radio, Peter Msechu amesema yeye pamoja na msanii mwenzake Banana Zoro hawachagui kazi, wanachoangalia wao ni pesa tu ambayo wataingiza.
“Kikubwa tu ambacho watu hawajui ni kwamba mimi na Banana Zoro hatuchagui, show yoyote ile hata ukisema nije niimbie kuku ambao unaona hawatagi, daktari akakwambia bwana hawa kuku wakipata bendi tu ya msechu hawa kuku wanataga, mimi nitawaimbia kuku kuanzia asubuhi mpaka jioni, ili mradi ni pesa tu kimsingi hatuchagui na tunafanya kazi nyingi”, alisema Peter Msechu.
SIku za hivi karibuni Peter Msechu alisikika akilalamika kuwa na hali mbaya kiuchumi na kusema pesa zote za muziki zipo kwa Diamond, hivyo inawapa wakati mgumu sana wasanii wengine kupata pesa.
eatv.tv