Picha: Mapokezi ya Rayvanny Akiwa na tuzo yake ya BET
Leo mchana kwenye majira ya saa tisa, msanii Rayvanny aliwasili nchini akiwa na tuzo yake ya BET ambayo aliinyakuwa usiku wa Jumamosi nchini Marekani aliwasili katika uwanja wa JK. Nyerere na kupata mapokezi makubwa kama ya kifalme.
Hitmaker huyo wa Mbeleko alipokelewa katika uwanja huo na mabosi wake wa WCB wakiongozwa na Diamond, Mkubwa Fella, Sallam pamoja na wasanii wenzake akiwemo Harmonize, Rich Mavoko, Queen Darleen na Lava Lava walioambatana na Bi. Sandra ambaye ni mama mzazi wa Diamond.
Msanii huyo aliongozwa na msafara mkubwa pamoja na mashabiki wake na kuanza kuitembeza tuzo hiyo katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, ikiwemo Buguruni, Kariakoo, Magomeni, Tandale, Sinza na Mikocheni.
Jionee baadhi ya picha za tukio zima