-->

Prof. Jay Afungukia Muziki wa Hip Hop Bongo, Awapa Makavu Wasanii Hawa

Rapa mkongwe nchini Prof. Jay ambaye mwaka jana alitoa ngoma ya ‘hip hop singeli’ iliyokwenda kwa jina la ‘Kazi Kazi’ ameibuka na kusema wivu wa baadhi ya wasanii wa hip hop Bongo hauwezi kusaidia muziki wa hip hop kufika mbali.

Prof. Jay

Licha ya wimbo huo wa ‘Kazi Kazi’ kufanya vizuri, na kuwepo kwa baadhi ya wasanii ambao waliupokea vizuri baadhi ya wasanii wa hip hop walionesha kutouelewa, huku wengine wakisema Prof Jay amekosea kutoa ngoma ya aina hiyo.

Prof Jay amesema wakati anatunga na kuandaa ngoma hiyo ya Hip hop Singeli alitambua wazi kuwa wapo watu wataipenda na wapo watu wengine hawataipenda, lakini kwa asiyeipenda kazi hiyo asilazimishe kila mtu kutaka kuichukia kazi hiyo.

“Kila mtu ana haki ya kupenda ambacho moyo wake unamwambia, tunakosea sana kutaka wote wapende kile tunachokipenda. Kupinga mtu aliyefanikiwa hakukupi uhalali wa wewe kufanikiwa, tuna nafasi ya kujirekebisha na kupeleka hip hop yetu mbali ila siyo kwa wivu” Prof Jay 

Prof Jay pia ameibuka na kujibu kile kilichosemwa na Nash MC kuhusu singeli kwenda kimataifa ambapo amesema kuwa watu wanaohoji hilo wanakosea sana kwani wao wanatakiwa kujiuliza kwanini muziki wa hip hop hauvuki ‘boda’ na kufika level hizo za kimataifa.

“Juzi tu dogo Nash MC aliuliza, eti kama tayari singeli imeshakwenda International? Nilitegemea angeuliza kwa nini hip hop  ya bongo haivuki boarder? Mkafurahia kishabiki bila kujiuliza hip hop ndiyo imezaa karibu aina zote za muziki wa kizazi kipya lakini mbona wasanii wake hawafiki mbali, matokeo yake baadhi ya wasanii wanaojiita wa Hip hop na mashabiki wao wanaichukia aina nyingine ya muziki kwa mafanikio wanayopata wenzao. Badala ya kujiuliza tumekosea wapi sasa tunakuwa na wivu wa kijinga na kuchukia mafanikio ya wengine waliopambana kufika hapo walipo sasa” alisisitiza Prof Jay 

Prof. Jay alizidi kusisitiza kuwa mapinduzi ya hip hop yaliofanywa na wasanii wa zamani yaliongozwa kwa upendo ndani yake na si chuki

“Mapinduzi yaliyofanywa na Kwanza Unit, Saleh Jabri, HBC, Sugu, Hashim, Majani, GWM, Solo, Afande, Jay Moe n.k yalifanikiwa kwa upendo siyo chuki, hata wanaojitahidi kupeperusha bendera ya  hip hop kama Fid Q, Joh Makini watu wanawakatisha tamaa, I RESPECT YOUR HUSTLE my young brothers. Matokeo yake hao wanaopinga wenzao
wanaoonesha juhudi, wanaishia kuimbia washkaji zao kwenye vibanda vya kahawa, You need to grow up”. Alisema Prof. Jay

Mbali na hilo Prof Jay amesema kizazi hiki cha hip hop kimekuwa kama kizazi cha kambale.

“Kizazi hiki cha hip hop kimekuwa kama ukoo wa kambale, yaani baba, mama na watoto wote wana ndevu, kila mtu akiambiwa mkali anajiona kweli kamaliza, hii heshima mliyoikuta kwenye hip hop tuliitafuta kwa jasho na damu, kisha mnaichukulia poa tu, badala ya kwenda mbele mnarudi nyuma kwa kasi”. Prof. Jay amemalizia 

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364