Prof Jay, Mwana Fa, Nash Mc Tunahitaji Vitendo Dhidi ya Maneno
MUZIKI wa Hip hop au Kemo kama unavyoitwa kitaalamu ni mama wa aina nyingi za muziki tunaousikia, umekuwa na mzuka wa aina yake kwa mashabiki hasa pale MC anapokuwa jukwaani akimwaga ladha ya mistari kwa mistari konde.
Nadhani asili na chimbuko lake ndiyo limefanya uwe muziki wenye amsha amsha kubwa tofauti na aina zingine za muziki japo kuwa kuna madai kuwa wasanii wake hawapo vyema kiuchumi.
Jambo hilo linafikirisha kidogo maana kama kweli Hip Hop haiuzi mbona wasanii wenye haiba ya Jay Z walitajirika kwa kuuza albamu na kanda mseto (Mix Tape) kwa kuzitandaza barabarani. Inawezekana kuna sehemu kwenye mfumo wa uuzaji wa kazi za Hip Hop kuna shida.
Kibongo bongo tumeshuhudia mpasuko baina ya marapa na ma Mc wanaodai kushika misingi ya muziki huo. Wale marapa wamefanikiwa kuliteka soko la Bongo Fleva kwa kuwa upande huo kwani msanii anaweza kunyumbulika kulingana na matakwa ya soko.
Lakini kwa wale wanaodai kufuata misingi hali zao kimuziki zipo vizuri ila kifedha sina uhakika kama wanalingana na walioamua kujichanganya na hapo ndipo majibizano kati ya Nash Mc, Profesa Jay na Mwana Fa ulipoanza huko kwenye mitandao.
Nash Mc aliuliza kwenye Facebook kuwa eti ile Singeli tayari imefika Intaneshino? Kauli hiyo ilimgusa Profesa Jay ambaye katika ngoma yake ya mwisho aliyofanya na Sholo Mwamba kuna mstari alisema tunaipeleka Singeli kwenda Intaneshino.
Profesa Jay akajibu kwa kusema nilidhani angeuliza kwanini Hiphop Bongo haivuki boda, badala ya kujiuliza tumekosea wapi, sasa tunakuwa na wivu wa kijinga kuchukia mafanikio ya wengine waliopambana kufika hapo walipo sasa.
Mwana Fan aye alifunguka kwa kusema “Chemsha Bongo, Bongo DSM, Jina Langu, Nikusaidiaje, Zali La Mentali, Promota Anabeep, Ndio Mzee, Hapo Vipi, Msinitenge, Niaminipaka nyingine nashindwa kukumbuka haraka”
“Come on man, hakuna mtu kwenye muziki wetu ana sifa za kumkosoa huyu ‘mzee’ tena kwa kumkosea adabu, sijui kwa nini wakati mwingine tunafanya tunayofanya, unatoa wapi vigezo vya kumuwakia mtu aliyeubadili mziki peke yake ukafikia kusikilizwa na rika zote nchi nzima?
Umeufanyia nini muziki cha kukupa wadhifa huo? come on, najua kuwa ‘muasi’ ni ‘sifa’ ya hiphop lkn tafadhalini muwe na viwango.
Profesa Jay, Nash Mc na Mwana Fa nyinyi wote mnajenga jengo moja, kutupiana maneno bila vitendo haisaidii kama unaona mwenzako amekosea fanya wewe kilicho sahihi.
Mtanzania