-->

R.O.M.A Mkatoliki Karudi, Makamuzi Yanaendelea, Sasa Yupo Fiti Kupanda Jukwaani (VIDEO)

RAPA kipenzi cha Watanzania, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amefunguka kuwa afya yake imeimarika na sasa yupo tayari kupanda jukwaani kukamua shoo kama kawaia yake.

ROMA ameyasema hayo leo wakati akitoa neno la shukrani kwa uongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Glopbal Publishers kwa kuendelea kumsapoti, kufanya naye kazi, kuboresha mahusiano yaliyo mema na kumfariji hasa katika kipindi kigumu alipopatwa matatizo ya kutekwa akiwa na wenzake watatu.

“Nimfika hapa kwa ajili ya kutoa neno la shukrani kwa jinsi ambavyo tmekuwa tukifanya kazi pamoja, pamoja na matatizo yaliyotukuta mimi na wenzangu lakini nyinyi Global Publishers mmeendelea kuwa na mimi katika kipindi chote hicho.

“Mtu akiona nimeweza kutembea kutoka nyumbani mpaka kufika hapa ofisini (Global PUblishers), basi ajue nipo fiti, na ninaendelea vizuri. kama nimeweza kushika maiki, nikazungumza basi hata Dar Live naweza kushika maiki (akimaanisha kufanya shoo).

“Niliona kipindi cha matatizo mlitupigania, magazeti ya Global Publishers yalifanya coverage nzuri na mlikuwa upande wetu. Kiukweli tulifarijika kuona watu wengi wakitutia moyo na kutupatia neno la faraja,”alisema Roma.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364