-->

Rayvanny awabwaga WizKid, Davido tuzo za African Act

Mmoja wa wasanii wanaounda lebo ya Wasafi (WCB), Raymond Shaban maarufu Rayvanny ametwaa tuzo ya African Act of The Year zinazotolewa na Uganda Entertainment Awards.

Kwa ushindi huo, msanii huyo amewabwaga Wizkid na Davido wa Nigeria na Vanessa Mdee wa Tanzania.

Rayvanny ameshinda tuzo hiyo ikiwa ni miezi michache tangu Juni 24, alipoandika historia katika tuzo kubwa za BET baada ya kuitwaa kwenye kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act 2017.

Msanii huyo kutoka Mbeya alianza kutikisa katika muziki baada ya kuibuka kupitia mashindano ya Free Style mwaka 2011. Aliachia singo ya kwanza iliyoitwa “Upo Mwenyewe” akiwa chini ya lebo ya Tip Top Connection.

Raymond alilamba dume alipokubali kujiunga na Wasafi ambako amerekodi nyimbo kadhaa ukiwemo “Natafuta Kik” na “Kwetu” ambao ulifanya vizuri sokoni.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364