-->

Roma Mkatoliki na Moni Watekwa!

Rapa Roma Mkatoliki ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Usimsahau mchizi’  msanii mwenzake na Moni Central Zone wamekamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana.

Roma Mkatoliki akiwa na Mona

Katika taarifa iliyotolewa na msanii Prof. Jay ambay pia ni mbunge wa Mikumi inasema msanii huyo alikamatwa jana akiwa studio.

Prof. Jay ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa jana wakiwa studio za Tongwe Records.

“Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua computer ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi” aliandika Prof. Jay

Kitendo cha rapper Roma Mkatoliki na Moni Central Zone kuchukuliwa usiku wa jana (Jumatano) wakati walipokuwa studio ya Tongwe Records na kupelekwa sehemu isiyojulikana, kimewaumiaza wengi. Zitto Kabwe na Nay wa Mitego ni miongoni mwa walioumizwa na tukio hilo.

Wawili hao wamekilaani kitendo hicho kupitia mitandao tofauti tofauti. “Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu zote,” ameandika Zitto kwenye Twitter yake.

Naye Nay kupitia mtandao wa Insytagram ameandika, “Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?! Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo ✊?✊?.”

Mpaka sasa bado hajafahamika wasanii hao wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi. Lakini watu kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364