Saida Karoli Atamani Collabo na Diamond
Msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amesema msanii Saida Kalori alimwambia kwamba anatamani kufanya naye kazi.
Diamond ameyasema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV ambapo ameweka bayana kwamba wimbo ‘Salome’ ambao unaendana kabisa na wa Saida Kalori ulipata Baraka zote kutoka kwake na walipowasiliana kwa njia ya simu alimwambia anatamani kufanya naye kazi.
“Sijabahatika kuonana naye ila niliongea naye kwa njia ya simu na akaniambia kwamba anatamani siku moja afanye kazi na mimi jambo ambalo ni jema” Amesema Diamond
Aidha Diamond amesema amefurahishwa na namna mashabiki kutoka ndani na nje ya nchi walivyoupokea vizuri na kusisitiza kwamba wimbo huo kutokana na mahadhi yake unafaa kupigwa katika nchi yoyote ndiyo maana mavazi yake yalizingatia tamaduni za makabila mbalimbali ndani na nje ya nchi ndani ya bara la Afrika.
eatv.tv