-->

Saida Karoli: Walioimba Wimbo Wangu Hawakunilipa

MWANAMUZIKI wa nyimbo za asili, Saida Karoli, amesema hajawahi kupokea fedha yoyote kutoka kwa wasanii waliorudia ama kutumia vionjo vya wimbo wake wa ‘Chambua kama Karanga’ tofauti na inavyodhaniwa na wengi.

Saida aliweka wazi suala hilo jana, alipotembelea Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, inayochapisha magazeti ya MTANZANIA, BINGWA, DIMBA na RAI, iliyopo Sinza Kijiweni, Jijini Dar es Salaam.

Karoli, anayetamba na wimbo wake wa ‘Orugambo’, huku akiwa mbioni kukamilisha albamu yake yenye jumla ya nyimbo 17, alisema alimpa Nasib Abdul (Diamond) ruhusa ya kurudia wimbo huo kwa kuwa aliamini ungemrudishia umaarufu wake na amefanikiwa lakini hajawahi kupokea fedha yeyote kutoka kwa Diamond wala msanii mwingine aliyerudia au kutumia kionjo cha wimbo huo.

“Mimi sikupokea fedha yoyote kutoka kwa Diamond, mimi nilimpa ule wimbo ili autumie kwa kuwa nilishafeli kwenye muziki, nikaona nikimnyima na mimi nilikuwa nimeshuka kisanii haitapendeza, nikaamua kumpa ili autumie labda utaweza kunitambulisha tena kwenye tasnia hiyo, kwahiyo hatukuwa na makubaliano ya kunilipa fedha kama ilivyokuwa ikivumishwa,

“Pia nia yangu kubwa haikuwa kupata fedha kwa kurudia wimbo huo, ila nilijua wimbo huo ukiimbwa na Diamond utapata nafasi kubwa na mimi umenirudisha, nashukuru na naamini nilipokosea sitarudia tena makosa ya kipindi hicho,’’ alisema Saida.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364