-->

Shilole Ashindwa Kufika Mahakamani Kutoa Ushahidi

Dar es Salaam. Msanii wa muziki wa kizazi wa Bongo Fleva na filamu, nchini Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameshindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi ya matumizi mabaya ya mtandao kwa kuwa anaumwa.

Zuwena Mohamed ‘Shilole’

Leo (Jumatano) Shilole alipaswa kutoa ushahidi katika kesi hiyo inayomkabili mwanafunzi wa Chuo cha Bandari, Thomas Lucas (20) inayosikilizwa mbele ya Hakimu Boniface Lyamwike.

Katika kesi hiyo, Lucas anakabiliwa na shtaka la mtandao kwa kumkashfu Shilole kupitia kwenye mtandao wa Instagram.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo alifanya hivyo wakati akijiua ni kosa na kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya mtandao namba 14 ya 2016.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17,2017 ambapo itaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364