Sijalivunja Jahazi- Said Fella
Meneja wa kundi la Yamoto Band, Said Fella amefunguka na kusema yeye si sababu ya kuvunjika kwa Band ya Jahazi Modern Taarab ambayo ilikuwa inamilikiwa na Mzee Yusuph baada ya wasanii wakongwe na nguli wa band hiyo kukimbilia kwenye Band mpya iliyoanzishwa na Said Fella.
Akizungumza kwenye eNEWZ Said Fella amedai kuwa yeye hajaivunja Jahazi bali wasanii hao wamekuja kwenye Band yake kwa lengo la kutafuta maisha na kufanya kazi ili watoto waweze kwenda shule.
“Mimi sijaivunja JAHAZI wale wamekuja na mimi nikasema sawa twendeni sababu mwisho wa siku wenyewe wanasema sisi tunapiga magitaa watoto wetu wasome na sisi tupate maisha, kwa hiyo la msingi na wewe unaweza kupata muda ukawatafuta wakina Mauji, Chid Boy, Bobu Ally, na wengine ukawauliza mbona mmefanya hivi wao watawambieni maana hayo ya kwako wao. Ila mimi najua Jahazi litaendelea kuwepo sababu ile ni Band kubwa na hawa kama wameamua kwenda kujitafutia basi sawa” alisema Said Fella