-->

Sijaona Wakumlinganisha na Alikiba – Harmorapa

Rapa ambaye amejizolea umaarufu sana kupitia mitandao ya kijamii Harmorapa amefunguka na kusema kwa Tanzania hii hajaona msanii wa kumfananisha na Alikiba na kusema hata ngoma yake ambayo amefanya na Juma Nature alitaka kufanya na Alikiba.

Harmorapa anasema kabla ya kurekodi ngoma yake hii mpya ambayo amefanya na mkongwa Juma Nature alijitahidi sana kumtafuta Alikiba ili aweze kufanya naye lakini jitihada zake ziligonga mwamba kutokana na ukweli kwamba Alikiba alikuwa na mambo mengi na kushindwa kumfikia kuzungumza naye jambo hilo.

“Kiukweli King Kiba kwa Tanzania hapa sioni wa kumfananisha naye, kwa hiyo nisema sijaona bado wa kumlinganisha naye sababu jamaa anafanya vizuri sana na anajua muziki sana, hata kabla ya kurekodi hii kazi yangu mpya nilifanya jitihada na watu wa karibu na Alikiba japo niweze kufanya naye kazi lakini sikuweza kufanikiwa kutokana na mambo yake kuwa mengi sana na watu pia ambao walikuwa wakinipa connection naye kuna vitu sikuweka sawa, na muda nikaona unazidi kwenda nikasema ngoja nifanye tu” alisema Harmorapa

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364