-->

Simu Yawagombanisha Vanessa na Jux

Msanii wa muziki wa bongo fleva Vanessa Mdee amefunguka na kuweka wazi kuwa mara nyingi huwa wanagombana na mpenzi wake huyo Jux kutokana na tabia yake ya kuchelewa kujibu jumbe fupi au hata kupokea simu zake.

Vanessa Mdee alisema haya kwenye kipindi cha ‘Ngaz kwa Ngaz’ kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana EATV na kudai kuwa Jux kwenye suala la simu amekuwa mvivu sana na ndiyo jambo linaloleta tofauti kati yao.

“Mvivu wa simu amefarakanishwa na simu yake huyu jamaa, hata kwenye kujibu txt au kupokea simu hana ushirikiano na simu kabisaa kwa hiyo tunagombanaga mara nyingi kuhusiana na communication” alisema Vanessa Mdee

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364