-->

Sipangiwi Wala Sifundishwi cha Kuongea – Nay wa Mitego

Msanii wa Bongo fleva Nay wa Mitego amefunguka mapya na kusema yeye hana muda wa kupoteza wa kupigana na msanii wa bongo ‘movie’ Yusuph Mlela huku akijitapa kuwa hapangiwi wala hafundishwi jambo analotaka kuongea.

Msanii wa Bongo fleva Nay wa Mitego

Nay ameeleza hayo baada ya kuambiwa na Mlela ajiheshimu na asiingilie kazi za watu ambazo hazimuhusu huku akisisitiza kwamba kama angekuwa anaimba basi angeingia studio ili atangeneze wimbo wa kumchana lakini kwa vile kazi zao haziingiliani alimtaka wapande ulingoni wazichape waweze kutengenezeana  heshima kati yao na siyo kupiga maneno tu.

“Mimi ni Baba mwenye watoto, mimi ni mtu  mwenye familia ‘so’ ukiwa unataka kuniuliza kitu angalia watu wa kuniweka nao ….Usiniweka na watu ambao unaona kabisa hiki siyo sawa. Mimi naongea na bongo ‘movie’ wote…Mimi nipo ‘free’ sana nipo huru kuongea jambo lolote…Mimi napenda kuongea ukweli, wewe unaweza kukataa nilichokiongea lakini asilimia kubwa wanaelewa ninachoongea ‘thats why’ nikisimama sehemu nikizungumza watu wanaelewa nazungumza nini, ndiyo maana sijawahi kupindisha, mimi huwa naongea ‘straight’ ndiyo maana kuna watu wananiamini sana ‘so’ sipangiwi, sifundishwi kwamba toa hiki weka hiki….Sina muda wa kupigana yaani sina muda kabisa”. Alisema Nay wa Mitego kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV.

Vile vile, Nay amesema uhuru aliokuwa ndiyo unamsababisha kuongea kila jambo analoliamini kwa upande wake kuwa lipo sahihi katika kipindi hicho huku akifafanua baadhi ya mambo kuwa yote aliyoyaongea alikuwa anawashauri wasanii wenzake bila ya kujali ni namna gani watakavyolipokea ili mradi yeye kaongea yake.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364