Sitatumia Tena Sumu Kuharibu Muonekano Wangu– Ray C
Msanii mkongwe wa muziki Ray C amedai ameupenda muonekano wake mpya huku akijipa mtihani wa kujizua kurudi katika mambo ambayo yalimpelekea kuupoteza muonekano wake mzuri wa mwili.
Muimbaji huyo hivi karibuni amekuwa akipost picha zake mpya ambazo zinamuonyesha akiwa na muonekano mzuri hali ambayo imewafanya mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kuona kweli mrembo huyo ana nia ya kubalika na kutoka katika matumizi ya Madawa ya kulevya.
Jumanne hii muimbaji huyo amepost picha yake katika mtandao na kuandika:Nimeanza kumpenda Huyu dada Ray C sitaki kumdhuru tena kwa sumu wala bunduki nataka Azidi kunivutia kila nimuonapo kiooni.
Kwa sasa muimbaji huyo anarekodi nyimbo zake katika studio ya Wanene Entertainment kufanya maandalizi ya ujio wake mpya.
Bongo5