-->

Siwezi Kuyarudia Matapishi – Mr Blue

Msanii wa Bongo Fleva Mr. Blue ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Mboga Saba’ amefunguka na kusema kuwa saizi yeye ni mtu mzima anaangalia maisha yake na familia yake hivyo hawezi kurudia matapishi ambayo tayari alishakwisha yatapika.

mr blu833

Mr Blue alisema haya kupitia kipindi cha eNewz ya EATV alipokuwa akifafanua juu ya taarifa zilizokuwa zimezagaa mtaani kuwa alimpigia simu aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Naj ndipo hapo aliposema hawezi kurudia matapishi aliyokwisha yatapika.

“Niliongea na Baraka The Prince alisema kuwa wao hawakufanya hilo jambo, lakini kama wangekuwa ni wao lazima ningetafuta njia ya kuwashikisha adabu maana huko ni kuharibiana. Mimi saizi nimeshakuwa mtu mzima siwezi kurudia matapishi ambayo nilishakwisha yatapika mwanzo’ alisema Mr Blue.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364