Snura Afungukia Ajali Yake!
SIKU chache baada ya kupata ajali mbaya, staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi amefunguka jinsi alivyonusurika kifo huku akimshukuru Mungu kwa kumtoa salama kwani mauti yalikuwa nje nje.
Awali, chanzo kilichokuwa eneo la tukio, kilieleza kuwa Snura alikuwa kwenye mwendo wa kasi na kushi-ndwa kukata kona iliyopo maeneo ya Cocacola Mikocheni na kusaba-bisha gari lake kupin-duka na kuu-mia sehemu mbalimbali za mwili wake.
“Ilikuwa ni ajali mbaya, kwa jinsi gari lilivyoanguka na kujibinua, ni wazi kuwa ile ni Mungu tu, vinginevyo hivi sasa tungekuwa tunasema mengine,” kilisema chanzo hicho.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Snura alikiri kupata ajali hiyo iliyotokea Ijumaa usiku wakati akiendesha gari lake akiwa na mdogo wake, lakini bahati nzuri hakuumia sana, zaidi ya kupata michubuko kwenye mkono na mdomoni.
“Unajua ajali ilikuwa mbaya sana, nashukuru waliotuokoa, chanzo cha ajali ni kwamba ile barabara siijui vizuri kwa hiyo sikujua pale kama kuna kona kali ndiyo maana nikapoteza mwelekeo.
“Kupona au kutoka hivi salama kwenye ile ajali ni Mungu tu, maana gari liliacha njia na kupinduka, lakini mimi na mdogo wangu tulipata michubuko midogo tu mwilini na sasa hivi tunaendelea vizuri tu,” alisema Snura.
Chanzo:GPL