-->

Snura Atoa Neno kwa Kichuya wa Simba

MSANII wa Bongo Fleva, Snura Mushi ambaye ni shabiki wa Simba, ameutazama mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 23 na kumtaka straika wao, Shiza Kichuya, kupambana na kuhakikisha anaitungua Yanga dakika za mwanzo.

Snura amekuwa akivutiwa na straika huyo tangu alipotua Simba na kuahidi kumsapoti kila wakati timu hizo zitakapokutana.

Akizungumza na MTANZANIA, Snura amemtaka Kichuya kufanya kweli kwenye mchezo huo huku akimwahidi zawadi endapo atafanikiwa kuwafunga wapinzani wao.

“Kichuya amekuwa shabiki wangu tangu alipojiunga Simba na amekuwa akiisaidia kwa kiasi kikubwa katika mechi zake, kikubwa ajipange na ahakikishe anawafunga hao mapema ili awaondoe mchezoni mapema,” alisema Snura.

Msimu uliopita mwanadada huyo alitimiza ahadi yake ya kumpa viatu vya mazoezi straika huyo baada ya kufanikiwa kuifunga Yanga mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi kuu.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364