-->

Soggy Doggy Atoboa Chazo cha ‘Kibanda cha Simu’

Msanii wa bongo fleva ambaye bado yupo kwenye game, Soggy Doggy, ametoa siri ya wimbo wake wa ‘kibanda cha simu’ ambao ulifanya poa sana miaka ya 2000, na kilichompelekea yeye kuandika wimbo huo ambao hauchuji masikioni mwa watu kwa ujumbe wake.

soggy34

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Soggy Doggy amesema chanzo cha yeye kuandika wimbo huo ni baada ya mama yake kupenda kufungia simu yao ya mezani ili kuogopa bili kuwa kubwa kwa watu kupiga hovyo, na kusababisha awe anakwenda kupiga simu kwenye vibanda vya simu, ambavyo kwa miaka hiyo vilikuwa kila kona ya mtaa.

“Kibanda cha simu ilianzia tuseme ni home, kwa sababu simu iliyokuwepo ilikuwa ni simu ya mezani, lakini mama muda wote ile simu, unajua simu za zamani zilikuwa zinapigwa kufuli pale, yani huruhusiwi kwenda kujipigia pigia tu masimu kwa sababu bili ikija itakuwa ni kubwa, kwa hiyo alichokifanya mama alikuwa anaifunga ile simu huwezi ukaenda tu mtu ukajipigia, kwa hiyo muda mwingi ilikuwa mi nikitaka kupiga simu ilikuwa inanilazimu niende kwenye vibanda nikapige simu, so nikiwa katika hivyo vibanda kupiga piga simu, nilikuwa naona ona hivyo vituko, yani huyu kaja amefanya hiki amefanya vile, so nikaamua kujiongeza kwenye kuandika, alafu nilikuwa naandika kama ni wimbo wa masihara”, alisimulia Soggy Doggy juu ya stori ya kibanda cha simu.

Soggy aliendelea kusema kuwa wimbo huo alitakiwa kushirikiana mwanamuziki wa kike ambaye kwa wakati huo alikuwa anafanya poa kwenye game ya Bongo Fleva, Rema Chalamila au Ray C, lakini alimtosa na ndipo akafanya na Josephine.

“Namshukuru Majani, Josephine aliyeshiriki, kwa sababu wimbo pia ulikuwa ni Ray C alitakiwa ashiriki, lakini Ray C hakujisikia ama aliona Soggy wa nini mimi, japokuwa Soggy ni kaka yake kwa mbali tu, ye akachukulia wa nini akakimbia kimbia, nashukuru Josephine nilimkuta studio hapo hapo, akashiriki kwenye wimbo na wimbo ukahit”, alisema Soggy Doggy.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364