-->

TID Afichua Rushwa Inavyowatafuna Wasanii

Mzee Kigogo ‘Mnyama TID’ amedai kuchukizwa na baadhi ya wadau wa muziki wanaowadai wasanii pesa ndipo ngoma zao ziweze kupenya kwenye masikio ya mashabiki kitu ambacho kinachangia kupotea kwa vipaji vingi mtaani.

Mnyama TID

Akiwa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio TID alidai wasanii wananyonywa na wadau wanaoshughulika kusukuma muzilki hali amabayo inawafanya wasanii wengi kutenga bajeti ya kufanya matangazo ya kutosha ili kazi ziweze kusikika mitaani na sehemu mbalimbali.

“Nakerwa sana na watu ambao hawajui jinsi gani sisi tunasumbuka. Unalipa studio, video na mambo kibao kwa ajili ya kufanikisha kazi, cha ajabu DJ anaweza akataka kupiga lakini mtangazaji anakwambia acha mpaka atoe kitu huu ni uuaji wa vipaji na ninapigana nao sana. Sasa wameshatujengea kwenye mindset kuwa ukiandaa ngoma andaa na pesa ya kutulipa ili kazi itembee”. TID alifunguka.

TID ameachia wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Woman’ na kudai ameamua kurudi tena kwani yeye ndiye msanii wa kwanza kutoka Tanzania kujulikana nchi za East Africa hivyo anataka kurudi tena kwenye ‘game’ kurudisha heshima yake.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364