TID amvaa Ben Pol kisa kuimba wimbo wake Fiesta Dar
Msanii wa Muziki wa Bongo Flava, TID amesema hajapendezwa na kitendo cha Ben Pol kuimba ngoma yake katika tamasha la ‘Fiesta’ wakati yeye hakuwa sehemu ya tamasha hilo.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo, East Africa Radio kuwa atazungumza na wakubwa wake pamoja na wanasheria wake ili kumchukulia hatua Ben Pol.
“Nina kesi moja na Ben Pol, huyo jamaa kwenye concert moja kubwa sana halafu ilikuwa na sponsored na wamemlipa hela nyingi lakini kwenye nyimbo zake alizofanya katika playlist yake kaweka wimbo wangu anaimba although those sponsor don’t like me kabisa because am not performing, am not there” amesema TID.
“Wao wanaimba unawalipa what about me, what about my copy right, ni makosa na nitaongea na wakubwa ila alichokifanya ni kuonyesha how is weak” ameongeza.
Alipoulizwa ni kiasi gani cha fedha anachohitaji kutokana na hilo, alijibu; baada ya kuongea na wanasheria wangu ndio nitajua, kwani yeye analipwa kiasi gani hadi anaimba wimbo wangu”.
Katika tamasha la Fiesta lilofanyika November 25, 2017 Dar es Salaam, Ben Pol baada ya kumaliza kuimba wimbo wake wa Moyo Mashine aliunganisha na wimbo wa TID ‘Nyota Yangu’.
Bongo5