-->

Ukweli Kuhusu Zawadi ya Gari Aliyoahidi Harmonize kwa Shilole

Utakumbuka mapema mwaka huu msanii Shilole alifanya harusi mara baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake, Uchebe. Mastaa kibao walimzawadia vitu mbali mbali, miongoni mwao ni Harmonize ambaye aliahidi kumnunulia Shilole gari aina ya Noah.

Hata hivyo Shilole amesema bado hajakabidhiwa gari hilo ila Harmonize kamdhibitishia kuwa ameshalinunua na kilichobaki ni makabidhiano mbele ya vyombo vya habari kama alivyokuwa akitoa ahadi hiyo.

“Ni kweli ameshaninulia tayari tunangoja tuweze kukabidhiana ile watu waweza kujua alichokihaidi, maana ukiwa umehaidi mbele ya kamera nitakuganda tu kwa sababu ahadi ni deni na sio dhambi,” Shilole ameiambia Clouds Fm.

“Ameniambia gari lipo tayari bado kukabidhi, mambo ya kuambiana vitu kwenye vyombo vya habari na kukabidhiana na ni huko huko, kwa sababu watu wameshaanza Shishi umepigwa sound hamna lolote nataka niwadhibitishe kuwa Harmonize hashindwi,” amesema.

Harmonize aliahidi gari lenye dhamani ya Tsh. Milioni 9 ili liwasaidie wawili hao katika shughuli zao za biashara. Shilole na Uchebe walifunga ndoa December 6 mwaka jana, 2016 na harusi yao ilifanyika January 14 mwaka huu.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364