‘Urugambo’ Inanikumbusha Mpenzi Wangu – Saida
Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili, Saida Kalori, ambaye kwasasa anatamba na wimbo wake mpya ‘Urugambo’ ametoa ya moyoni kuwa wimbo huo unamkumbusha mpenzi wake wa zamani.
Saida anasema umaarufu wa wimbo huo umemsababishia kero kwa midume wakware ambao kila kukicha wanampigia simu.
Hata hivyo Saida amesema hataki kuwasikia kwani amechoshwa na tabia za wanaume wanaomfuata kwa malengo yao kisha humtema mara wanapofanikiwa malengo yao.
Alisema ni bora amtafute mpenzi wake wa zamani ambaye kila anapomfikiria anaumia kutokana na mapenzi mazito aliyonayo kwake.
Saida alianza kuwa maarufu miaka ya mwanzao ya 2000, baada wimbo wake ‘Salome’ kuwa maarufu ndani na nje ya nchi.