-->

Ushauri wa King Crazy GK kwa Diamond Platnumz

Rapa mkongwe katika tasnia ya muziki wa Bongo King Crazy GK amefunguka na kutoa ushauri kwa msanii Diamond Platnumz na kumtaka kuwa na kitu kingine kwa sasa nje ya muziki kwa kuwa muziki una kawaida ya kupanda na kushuka.

gk94

Amesema hiyo itamsaidia endapo ikitokea muziki umeshuka upande wake, aendelee kunufaika na kuingiza pesa kwa miradi mingine ambayo inamfanya azidi kuwa juu siku zote katika maisha.

King Crazy GK alisema haya alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo na kudai biashara ya muziki ina kupanda na kushuka hivyo kwa jina alilonalo saizi Diamond Platnumz anapaswa kulitumia kufanya biashara nyingine nje ya muziki ambayo inaweza kumuingizia pesa zaidi ili hata siku muziki ukibadilika maisha yake yaendelee kubaki juu.

“Diamond Platnumz saizi anahitaji kuwa na kitu tofauti na muziki kwani muziki siku zote una kupanda na kushuka, kwa jina alilonalo sasa anaweza kuingiza pesa nyingi sana kama atalitumia vizuri, anaweza kuandaa ‘Proposal’ nzuri akawafuata watu kama kina Mo Dewji akatengeneza maji ya kunywa yenye nembo yake kisha akapata asilimia kadhaa kwenye maji hayo, yaani biashara zipo nyingi anaweza kufanya nje ya muziki ambayo itampa pesa nyingi zaidi, maana kutegemea muziki pekee siku muziki ukishuka inaweza kuwa tatizo” alisema GK

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364