Uwoya Alinitaka Mwenyewe – Msami Baby.
Mwanamuziki anayefanya poa na ngoma ya ‘So Fine’ Msami baby amedai hana mawazo ya mpenzi wake wa zamani, msanii wa bogo movie, Irene Uwoya kutoka kimapenzi na msanii Dogo Janja kwani hakuwahi kumtaka bali mwanadada huyo ndiye aliyemtaka wa kwanza.
Msami amefunguka hayo kwenye FNL ya EATV ijuma hii wakati alipokuwa akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho kuhusu kupotea kwake kwenye game kama kumechangiwa na mawazo ya mapenzi.
“Dogo Janja kutoka kimapenzi na Irene haijanishangaza au kunifanya mimi nipotee kwenye game kwa sababu kwenye mapenzi mimi sijawahi kuachika bali huwa naachaga. Uwoya yeye ndiye alinitongoza mimi kwani sijawahi kumtongoza ……..”. Kuhusu kuwa kimya ukweli nilipata ajali ya kuvaana na gari uso kwa uso kwa hiyo nilikuwa najiuguza kwanza, Ajali yangu haikusababishwa na ‘stress’ za mapenzi kabisa”. Msami baby alifunguka.
Msami baby aliwahi kutajwa miaka miwili nyuma kujihusisha kimapenzi na diva huyo wa bongo movie huku akidaiwa kumtelekeza mpenzi wake na baada ya hapo pia alitajwa sana kujiweka kwenye mapenzi na muigizaji Kajala.
EATV.TV