-->

Vanessa Penzini Tena?

Msanii wa kike bongo kwenye game ya bongo fleva anayekimbiza kimataifa Vanessa Mdee, ameonekana kupata mbadala wa aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu Juma Jux, kwa kuanza kumposti mwanaume mwingine huku kukiwa na ‘caption’ zenye ujumbe wa mahaba.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram siku chache zilizopita Vanessa Mdee alimposti msanii wa Nigeria Run Town na kuandika ujumbe wenye utata kwa hali ya kawaida, huku mwenye we Run Town akijibu kwa kuandika ‘Nakupenda babe’.

Lakini pia msanii huyo wa Nigeria alimposti Vanessa Mdee kumtakia heri kwenye siku yake ya kuzaliwa ambayo ilikuwa mwezi wa 6 na Vanessa kujibu kwa ujumbe wa mahaba, na pia Vanessa alimuweka Run Town na kuandika ujumbe mtamu na kisha Runtown kurudisha majibu kwa ujumbe mtamu zaidi wa mahaba.

Hivi karibuni Vanessa Mdee ameweka wazi kuwa hayupo kwenye mahusiano yoyote kwa sasa huku akiweka wazi bado ana hisia juu ya mpenzi wake zamani Juma Jux, lakini kwa sasa inaonekana mambo yameenda sawa na kumpata mbadala wake.

EATV.TV

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364