-->

VIDEO: Dayna Atetea Picha Zake za Utata Mitandaoni

Msanii wa bongo fleva Dayna Nyange amesema hawezi kuishi maisha ya kumfurahisha kila binadamu bali anaishi kama vile jinsi anavyoona inafaa kwa upande wake ndiyo maana haoni kama kuna tatizo la yeye kuwa na picha za utata katika mitandao.

Wakati akihojiwa na kipindi cha eNewz cha EATV leo kutokana na picha zake za utata zinazomuonesha sehemu zake kubwa ya mwili alizotupia katika mitandao ya kijami, Dayna amesema kuwa kuna vitu vinamlazimu yeye kuwa na picha za aina hiyo ikiwa ni pamoja na kazi yake.

Aidha Dayna ameongeza kuwa kuna watu wanapenda kutazama picha za aina hiyo ndiyo maana wengine wamehifadhi picha kama zake za wasanii wa nje katika simu zao, hivyo yeye kuwa na picha za aina hiyo, isiwashangaze watu na kama kuna watu ambao hawazipendi waache kumfuatilia ili wasizione.

“Mimi mama yangu hayupo katika mitandao ndiyo maana hazioni picha hizo, na wakumbuke kwamba wanayemuona kwenye picha hizo ni Dayna wala siyo Mwanaisha Nyange ambaye ni mama wa mtoto mmoja” Alisema Dayna.

Hata hivyo mrembo huyo anayetamba na ngoma yake mpya ya ‘Komela’ ameongeza kuwa picha za utata alizopiga pamoja na zile alizopiga akiwa na nguo za kuogelea ni za kawaida na kwamba mpaka anafikia uamuzi wake wa kwenda studio alikuwa na akili timamu na hakuzipiga kwa bahati mbaya.

Tazama interview aliyofanya na eNewz

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364