-->

VIDEO: Nimemsamehe Baraka – Ben Pol

Mwanamuziki wa miondoko ya RnB bongo, Ben Pol amejibu ‘diss’ ya Baraka The Prince kuhusu ujio wa wimbo wake mpya na kusema kuwa amesha msamehe siku nyingi, kabla hata hamjamkosea huku akiongeza kwamba anajitahidi kumsaidia msanii huyo akue.

Ben ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV na kusema anafahamu kuwa baadhi ya vitu haviko sawa kwa Baraka ndiyo maana hashangai hata akiwa anamkosea na kuiponda kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la tatu.

“Baraka mimi nilishasemaga nimemsamehe hata kabla hajanikosea, sisubiri anikosee ili nimsamehe hata siku moja kwa kuwa kuna vitu najua haviko sawa kwake….Kwa hiyo nimeshasema sijishughulishi nategemea chochote kile kutoka kwake” alisema Ben Pol.

Pamoja na hayo, Ben aliendelea kufunguka kwa kusisitiza baadhi ya mambo kwa kusema “Baraka ni mdogo wetu tunamsaidia pia akue…..hatujatengana kabisa na Baraka yaani hakuna utengano wowote. Mimi na Jux ndiyo tuliwaza mwanzo tuanzishe umoja flani tuwe tunafanya ‘shows’, tuna invite marafiki zetu wanatu-join tunafanya nao kazi ambapo tumeshamu- win Baraka, Vanessa, Joh Makini’ – Ben Pol aliongeza

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364