-->

VIDEO: Shaa Afunguka Kuhusu Kolabo na Chipukizi

Malkia wa uswazi anayefanya poa kwenye game ya bongo fleva, Shaa amefunguka na kusema haoni shida kumsaidia msanii chipukizi ili kutimiza malengo yake kwani hata yeye alishikwa mkono na wasanii wakubwa pasipo kulipishwa hata shilingi mia.

Shaa

Akiongea kwenye kipindi cha FNL cha EATV, Shaa amesema yeye wakati anaanza muziki akiwa msanii mdogo aliweza kupata nafasi ya kumshirikisha AY kwenye wimbo wake ‘Pambazuka’ bila hata ya kudaiwa hela na msanii huyo, hilo ndio limempelekea kuvutika kufanya kitu kama hicho ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila.

“Nilipokuwa mikoani nafanya media tour nilikutana na wasanii wengi wakali nikafanya nao kolabo ikiwa pia ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa watu wangu, kutokana kuwa hata mimi AY alinishika sana mkono nikiwa sijamlipa hata mia hivyo na mimi nitaendelea kufanya hivi,” Shaa alisema.

Baadhi ya nyimbo ambazo muimbaji huyo amefanya na wasanii chipukizi ni ‘Nikilewa’ wa Nasi kutoka Iringa, na ‘Mali ya Mungu’ wa Biznea kutoka Mwanza na nyingine.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364