VIDEO : Snura Awakanya Wasanii
Muimbaji na muigizaji bongo, Snura Mushi amewakanya vijana wanaotaka kuingia katika tasnia ya sanaa waepukane na vishawishi vya kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya huku akidai kufanya hivyo hakufanyi uonekane unaenda na wakati.
Snura amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz baada ya kutuhumiwa akijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinamfanya kumpa mizuko ya kufanya vizuri pindi akiwa stejini akitumbuiza.
“Vijana wenzangu kama mnaingia kwenye sanaa achaneni na vishawishi, kuna vishawishi vya kipumbavu sana, eti uonekane unaenda na wakati na ndiyo vinawaponza watu wanaingia kwenye dawa za kulevya huko wanavuta bangi eti mtu apate stimu afanye kazi vizuri nani kakwambia ?, mimi napanda kwenye steji situmii kilevi cha aina yeyote Mungu wangu aliyekuwa mbinguni ni shahidi sinywi pombe sivuti na nina panda kwenye steji nafanya vizuri tu kiasi kwamba wewe unaweza kufikiri nimetumia kilevi kwa sababu akili yangu nimeijenga kwamba hii ni kazi” alisema Snura