-->

VIDEO : Young Dee Amkana Mama wa Mtoto Wake

Msanii Young Dee a.k.a Pakarasta amemkana mzazi mwenzake Mamisa na kusema hakuwahi kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi japo kuwa wamepata mtoto kama baraka tu kwake.

Young Dee amesema hayo kupitia kipindi cha 5 Selekt cha EATV na kudai kitendo kilichotokea hakikuwa katika mipango yake hivyo sasa hivi kila mmoja ana maisha yake.

“Am single and am busy’, sina mahusiano, ni kitu ambacho naweza kusema kibinadamu kinatokea kama baraka tu kwa sababu hakuwahi kuwa mpenzi wangu na imebaki kama ilivyokuwa mwanzoni” alisema Young Dee.

Katika upande mwingine, Young Dee amedai yupo mbioni kuachia wimbo wake mpya ambao anaamini utakuwa mkali zaidi ya ‘Bongo bahati mbaya’  huku akisistiza kuwa ataendelea kufanya kazi na mtayarishaji wa muziki bongo Mr T- Touch

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364