VIDEO:Kutumia Ushirikina ni Sawa – Sam wa Ukweli
Msanii Sam wa Ukweli ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake wa ‘Kisiki’ amefunguka na kusema ushirikina kama ukiutumia vyema kwa ajili ya mambo yako ya faida kama kazi zako au ya kimaendeleo ni sawa.
Sam wa Ukweli amesema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha 5Selekt na kusema kama una utumia vyema uchawi kwa ajili ya mambo yako ni sawa ila si sawa kama unautumia uchawi au ushirikina kuwaumiza watu au kuwakwamisha watu katika mambo yao ya kila siku.
“Kama unautumia ushirikina katika mambo yako ni sawa lakini siyo kuutumia ushirikina kuwaumiza watu wengine, kitu chochote unachokifanya lazima kiwe na faida kwako si unaona sisi binadamu huwezi kutegemea jambo moja ndiyo maana kuna usiku kuna mchana, kuna asubuhi kuna jioni, kuna yes na kuna no, sasa mwingine anatumia ushirikina kukandamiza wengine wasifanikiwe” alisema Sam wa Ukweli
Tazama video hii Sam wa Ukweli akifunguka zaidi juu ya jambo hilo.