-->

VIDEO:Wasanii Wanaotuhumiwa Kujihusisha na Madawa ya Kulevya Wafikishwa Mahakamani

Takriban watuhumiwa 10 wa dawa za kulevya ambao ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi hii.

Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani sasa ni wasanii Rommy Jones, TID, Babuu wa Kitaa, Nyandu Tozzy, Tunda (model wa kike), Lulu Diva, Recho, Joan, na wengine.

Watuhumiwa wote wamesomewa kiapo cha Mahakama ambapo awali upande wa Jamuhuri uliomba watuhumiwa hao waamrishwe kuwekwa chini ya uangalizi kwa kuripoti polisi mara 2 kwa mwezi kwa kipindi cha miaka 2 ili kuangaliwa kama wameacha tabia ya kutumia dawa hizo hususani bangi.

Wakili wa upande wa utetezi Albert Msando anamedai taarifa hizo hazijakamilika kwani hazioneshi wanaojiusisha na dawa za kulevya na walikamatwa lini na wapi na hakuna ushahidi wa kujitosheleza wa madai hayo kiasi cha wao kupata dhamana ya kuangaliwa tabia zao bila polisi kutoa ufafanuzi wa kina wa kwanini wanahitaji kupata dhamana ya uangalizi wa nidhamu.

Baada ya hoja za pande zote mbili, maamuzi yakatolewa….

Akitangaza maamuzi ya mahakama, Hakimu Mkuu Huruma Shaidi amesema mahakama inawaamuru wajibu maombi kuwekwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha muda wa mwaka mmoja na kutakiwa kuwasilisha bondi ya shilingi milioni 10 kila mmoja bila mdhamini, ili wape dhamana

Watuhumiwa hao wote wanashughulikia suala la dhamana, na endapo watakamilisha wataachiwa kwa dhamana.

Wakati watuhumiw hao wakiendelea kushughulikia dhamana, kundi lingine la wasanii watano wanaotuhumiwa kwa dawa za kulevya wakiongozwa na Petit Man wamefikishwa katika mahakamana hiyo

Taarifa zaidi zinakuja, enedelea kufuatilia hapa.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364