Wamevujisha Wimbo Kuniharibia – Q Chief
Mkali wa Rnb na Zouk Tanzania Q Chief amefunguka na kutoa malalamiko yake kwa baadhi ya watu ambao wamevujisha wimbo wake mpya kwa lengo la kumuharibia soko la muziki wake kuuza katika njia za mitandao.
Q Chief muda mrefu alisema ameshafanya kazi na msanii kutoka nchini Nigeria Patoranking na kuanza promo kama maandalizi ya kutoa wimbo huo, lakini leo asubuhi wimbo wa msanii huyo ulianza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii na katika blog mbalimbali jambo ambalo limemfanya msanii huyo kufunguka na kusema wimbo huo ‘Original version’ bado haijatoka na wasubiri kupata maelekezo kutoka kwake ya namna gani wataipata.
“Morning wadau naomba niwajuze kwamba wimbo wangu mpya wa ‘Koku’ Q Chief ft Patoranking bado haujatoka ila kuna mtu mmoja ameamua kuivujisha kwenye mitandao kwa lengo la kuniharibia nawaomba msipotoshwe ‘Original version soon at Mkito Inshaalah Mungu ataweka mikono yake” aliandika Q Chief
eatv.tv