-->

Wanatumia Ndumba Kunipoteza – Sam wa Ukweli

Msanii Sam wa ukweli ametuma salam kwa wasanii wenzake wanaomfanyia fitina kwa kutumia ndumba asirudi kwenye muziki waache kwani tayari ameshawafahamu na kuwataka wasiogope yeye kurudi kwenye ‘game’ kwani kila mtu ana riziki yake.

Akifunguka kwenye eNewz ya EATV, Sam wa Ukweli anayetamba na ‘hit’ ya Kisiki amedai kuwa amepewa taarifa na baadhi ya watu kuwa wasanii wenzake huwa wanachinja hadi kondoo huku wakitaja jina lake ili kumpoteza.

“Wakikaaga vikao mimi kuna watu wananipenda katika kamati zao kwa hiyo wakimaliza wananipigia simu oyaa leo wameangushwa wanyama saba mara kuna mganga kutoka Kigoma kaletwa jiweke vizuri, Sasa nashangaa kwa nini hawataki mimi nirudi wakati watanzania wanatakaa kunisikia huu ni wakati wangu waniache” Sam alijinadi.

Msanii huyo ambaye amedai wimbo wa ‘Kisiski’ aliuachia tangu mwezi wa kumi mwaka jana bila video na kwanza amesema alipata changamoto nyingi katika kuandaa video yake kitu ambacho binafsi amedai imesababishwa na fitina za ‘ndumba’ na kwamba kuna watu waliotaka kumfelisha.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364