-->

Witness ‘Kibonge Mwepesi’ Afungukia Wasanii Kuibiwa Nje

Msanii wa Muziki Bongo, Witness amedai kuwa wasanii wengi wanaibiwa kazi nje ya nchi kutokana hamna mfumo wa kufutilia.

Muimbaji huyo amedai kutokuwepo kwa utaratibu wa kuwalipa wasanii mirabaha hapa nchini kunawafanya wengi wao kushindwa kufuatilia kitu kama hicho nje ya nchi.

“Uhakika upo wasanii wengi wanapigwa nje ya Tanzania hawajui namna gani ya mapato yao kuyakusanya. Kwanza kabisa kwa kuanzia endapo radio station na tv station za hapa Tanzania hawalipi hiyo mirabaha maana yake wale pia hawawezi kutuletea sisi zile fedha,” Witness ameiambia Bongo5 na kuongeza.

“So wanacho-assume ni kwamba kutokana na sheria ilivyo wale wanamuziki wa nchi nyingine ambao wanapaswa kulipwa zile pesa na hawajafika kwenye makubaliano ya makabidhiano wanaenda kuwapatia watoto wa nchi hiyo hizo fedha,” amesema.

Witness ni miongoni mwa wasanii walioteuliwa kuingia katika kamati ambayo itajadili namna ya kubadili mfumo wa sasa na kuleta ambao utawanufaisha wasanii na kazi zao pamoja na kutatua changamoto zao.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364