Young Dee Aeleza Sababu ya Kufanya Video na Tunda
Rapa Young Dee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Furaha’ amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa iliyompelekea yeye kufanya kazi na mwanamitindo Tunda.
Young Dee akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio alisema kuwa aliamua kufanya video hiyo na Tunda kwa sababu kwanza ni mtu ambaye yupo naye karibu hivyo kwake haikuwa kazi ngumu kumuitaji lakini pia adai alikutana na wanamitindo wengine ambao kwake walikuwa wakubwa sana akamua ngoja afanye na mtu wake wa karibu.
“Kwanza unajua sijafanya muda mrefu video ya mapenzi, hivyo nilifikiria nikaona Tunda ni mtu sahihi kwanza ni mtu wangu wa karibu hivyo nikaona akisimama yeye kwenye video hii ataleta maana zaidi kwa kile nilichokuwa nimelenga kukifikisha kwa jamii, maana nilikutana na wanamitindo wengine kwangu walikuwa wakubwa sana. Lakini pia nikiwa na Tunda muda wote kwangu ni furaha tu” alisema Young Dee.
Mbali na hilo anadai kuwa kipindi ambacho aliachia wimbo wake wa ‘Hands up’ ni kama alikuwa amewahi sana kwani alikuwa anajiona anahitaji kupumzika kwanza, kujijenga upya ili kuingia kwenye ushindani kweli na kufanya kazi rasmi.
“Kipindi kile kiukweli niliwahi sana maana tulikuwa na mizuka sana lakini kuna siku nilipost picha Instagram mimi mwenyewe nilijiona nimekonda kweli, nikaona nahitaji kupumzika, kulala vizuri na kufanya mazoezi ili nikirudi nirudi kweli ndiyo kama sasa nipo fiti kwa ushindani ndiyo maana nimekuja na hii kazi ya ‘Furaha'” alisema Young Dee
eatv.tv