Young Dee Aomba Radhi Kuhusu Picha ya Utupu
Rapper Young Dee amewaomba radhi mashabiki wake kutokana na picha ya utupu iliyosambaa leo mitandaoni , akiwa na Amber Lulu ambaye ndiye aliyekaa utupu.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Young Dee ameandika kwamba picha hiyo imevujishwa na watu wasiojulikana, ambayo ilikuwa na lengo la tangazo la nguo.
“Nasikitishwa kwa picha inayosambaa mitandaoni.. imevuja bila ridhaa yangu ni picha iliyokua imepigwa ‘behind the scene’ lengo haswa la ‘photoshoot’ ni aina hii mpya ya mavazi ya aina ya ki”Scortish” kama sketi. Naomba radhi sana kwa hili! na kwa mashabiki wote”, aliandika Young Dee.
Picha hiyo ambayo imesambaa kwa kasi sana kwenye mitandao ya kijamii imeonekana kushtua watu wengi kwenye mitandao, na haifai kuwekwa wazi.