-->

Young Killer Akubali Yaishe

Yale majibizano kati ya Nay pamoja na Msodoki yameendelea tena, baada ya Nay wa Mitego kusema amesikia ngoma ya Young Killer lakini kwake ni kama jingo kwani wimbo huo haujamilika. Msodoki amekiri ‘True Boya’ si wimbo rasmi kwani hakufanya serious.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Young Killer amesema wimbo wake huo ambao aliutoa rasmi kwa ajili ya kumjibu Nay wa Mitego amekiri si wimbo rasmi kwake ndiyo maana hakuwa serious sana katika ngoma hiyo na kusema wimbo wake rasmi unakuja muda si mrefu.

“Kwanza mimi sijafanya serious wimbo wangu ‘True Boya’ kwa sababu sijauandaa kwa muda mrefu sana ni wimbo nilioundika kwa masaa mawili tu nikaingia studio nikarekodi ndiyo maana kimekuwa ni ki verse kimoja tu, kwa hiyo siyo wimbo wangu rasmi lakini ni wimbo ambao nahitaji upigwe na uendelee kusikika kwa sababu ni wimbo ambao unakila sifa ya kusikilizika na kupendwa kwa kila kile nilichokifanya japo sikuwa ‘serious’ ” alisema Young Killer

Mbali na hilo Young Killer amedai kuwa wimbo wake rasmi ambao amefanya na msanii Harmonize utatoka baada ya wiki mbili kutoka sasa na kuwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kusikiliza ngoma hiyo ambayo mwenyewe anaamini kuwa italeta shida mtaani.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364