-->

Monalisa kuipeleka tuzo ya APA Bungeni

Dar es Salaam. Siku mbili baada ya msanii Yvonne Cherrie ‘Monalisa’, kuibuka msanii bora wa kike katika tuzo za za African Prestigious Awards (APA), anatarajia kuipeleka tuzo hiyo Bungeni kesho.

Utoaji wa tuzo hizo ulifanyia Aprili 14, mwaka huu Accra, Ghana ambapo lengo lake ni kutambua maendeleo na tija aliyonayo mtu kwenye nyanja za uongozi, biashara, sanaa na kadhalika.

Taarifa kutoka kwa mama yake, Susan Lewis ’Natasha’ iliiambia MCL Digital leo kwamba baada ya msanii huyo kutua leo asubuhi, kesho anatarajiwa kwenda mjini Dodoma kwa mwaliko wa kuipeeka tuzo hiyo bungeni.

Monalisa kupitia ukurasa wake mtandao wa kijamii wa Instagram, amewashukuru watanzania kwa namna walivyoweza kumpigia kura.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Monalisa amesema” Tuzo ni ya kwenu, mmekuwa nami kwa zaidi ya miaka 19 ya kazi yangu ya Sanaa hamjaniacha mnaendelea kunifurahia nashukuru mno mno, ahsante kwa muda wako uliotumia kunipigia kura.

Katika kipengele hicho cha muigizaji bora wa Kike, Mona alikuwa akichuana na wasanii maarufu wa kimataifa akiwemo Lupita Nyong’o ambaye ni mwigizaji wa Hollywood mwenye asili ya Kenya na Jack Apia mwigizaji kutoka nchini Ghana.

Waigizaji wengine waliong’aa kwenye tuzo hizo mbali na Monalisa ni Vicent Kigosi ’Ray’ aliyeshinda kipengele cha muigizaji bora wa kiume na Moise Hussein aliyeshinda kwenye kipengele cha mpiga picha bora barani Afrika kwa mwaka 2017.

Hata hivyo; mchekeshaji maarufu, Omar Athuman ’Mzee Majuto ‘ aliyekuwa akiwania kipengele cha cha mchekeshaji bora bahati haikuwa yake.

Kutokana na ushindi huo, sasa Monalisa ndio mwigizaji bora wa kike Afrika kupitia tuzo hizo za (APA).

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364