-->

Wolper Afunguka kuachana na Brown

Msanii Jackline Wolper ambaye hivi karibuni amekumbwa na tetesi za kuachana na mpenzi wake, amekanusha taarifa hizo na kusema kwamba wakiachana mashabiki wake watajulishwa.

“Watanzania wamezoea sana Instagram, usipompost bwana wako basi mmeachana, hawajui hata kama watu mumepata deal, mmeingia mikataba, hautakiwi kuweka mapicha ya mapenzi, mpaka wanataka utoe siri sasa, kuna issue siwezi kuiongelea, hivyo hakuna kitu kama hicho kikiwepo nitaongea”, amesema Wolper

Wolper amekutwa na tetesi za kuachana na Brown  baada ya kuonekana akishikana mkono kusalimiana na x wake, kwenye sherehe ambayo wawili hao walihudhuria.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364